24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Arthur hatarini kuikosa Copa America

PORTO ALEGRE, BRAZIL

KIUNGO wa timu ya taifa ya Brazil, Arthur Melo, yupo hatarini kuikosa michuano ya Copa America baada ya juzi kuumia goti kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Honduras, huku Brazil ikishinda mabao 7-0.

Kiungo huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Barcelona, alipata maumivu hayo katika dakika ya 29 baada ya kuchezewa vibaya na Romell Quioto ambaye alioneshwa kadi nyekundu moja kwa moja.

Copa America inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa wiki hii huku Brazil wakiwa wenyeji wa mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu 12 kutoba bara la America Kusini.

Uongozi wa timu hiyo umedai kuwa, hadi sasa haujui mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, lakini wanasubiri vipimo kutoka wa madaktari.

Nyota mwingine wa timu hiyo ambaye anatarajia kuikosa michuano hiyo ni pamoja na Neymar Jr ambaye wiki iliopita alichanika enka kwenye mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na michuano hiyo, hivyo hatuweza kuungana na kikosi hicho kwenye michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles