22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

AMBER LULU, LULU DIVA HAWATAFANIKIWA KUIUA BONGO FLEVA

Na RAMADHANI MASENGA

AMBER LULU na Lulu Diva ni miongoni mwa Video Vixen maarufu sana. Katika miaka ya hivi karibuni kufanya kazi hiyo siyo shughuli kubwa sana.

Binti anahitajika kuwa na sura yenye mvuto na umbo la kutamanisha. Kisha atupie picha za hovyo mitandaoni. Amber Lulu, Lulu Diva na Gigy Money wamefanya hivyo.

Pia Masogange japo hakuanza hivi ila pia naye kafanya haya. Ni vigumu sana kutenganisha u video vixen na utovu wa maadili.

Kati ya mavideo vixen wengi waliopo, ni wachache wenye kujitunza na kujiheshimu. Labda hawafiki hata watatu. Sasa baada ya kutamba katika video za wasanii wengine, Amber Lulu na Lulu Diva wameugekia muziki.

Kila mmoja katoa ngoma yake na video juu. Nyimbo zao zinatamba. Siku hizi mabinti warembo hawataki tena kuigiza kama ilivyokuwa zamani.

Siku hizi kama siyo u-video Queen basi wanaimba muziki. Wengi wao siyo wasanii hasa. Hawaitambui sanaa na miiko yake.

 Wasikilize hata katika mahojiano yao utagundua mtihani uliopo vichwani mwao. Katika moja ya mahojiano aliyofanya Amber Lulu ameacha watu midomo wazi.

Alipoulizwa kuhusu aina ya mwanaume anayemtaka, alijibu yeyote tu yeye sawa. Yeyote hata kama ni chizi yeye sawa. Ilimradi awe na uwezo wa kumtunza na kuujali mwili wake.

Hataki mambo mengi. Hata liwe jizi, jambazi au uaji yeye sawa tu. Hataki mwanaume mwenye kujiheshimu wala sifa njema katika jamii.

Hataki mwanaume makini ama mwenye kujali na kuilinda heshima yake katika jamii. Yeye ni mwanamume mwenye hela tu.

Aliyesema maneno haya sasa anaimba muziki. Kwa hiyo naye ni msanii hivyo ni kioo cha jamii. Kupitia kauli yake unaweza kujua Amber Lulu ni mtu wa namna gani.

Ila siyo kauli tu inayomfunua Amber Lulu. Hata picha zake nyingi katika mitandao ya kijamii zinaonesha yeye ni mtu wa namna gani.

Ni aibu kumwita na yeye ni msanii. Kumwita hivyo ni kuwakosea heshima kina Ditto, Lady Jaydee, Amini na wengine.

Amber Lulu ni miongoni mwa wazugaji wengi walioamua kujificha katika sanaa. Aina hii ya watu, ilivamia Bongo Muvi na kuiacha ikiwa mahututi.

Kama Bongo Fleva isingekuwa imekomaa, kwa ujio wa kina Amber Lulu basi ingeenda ilipo Bongo Muvi. Bahati kwa Bongo Fleva ni kwamba japo kina Amber Lulu ni maarufu ila hawana ustaa katika muziki.

Hii ni tofauti na ilivyokuwa Bongo Muvi. Kina Wema Sepetu japo hawakuwa na uwezo wa kina Riyama na Monalisa ila walikuwa mastaa zaidi ya wao.

Wema anapokuwa staa katika tasnia yako huna unachoweza kufanya zaidi ya kusubiri mauti ya jambo lako. Ndivyo ilivyokuwa katika Bongo Muvi.

Amber Lulu na wenzake ni watu wa matukio na siyo wasanii. Unapowapa nafasi kubwa sana katika jukwaa na kuwasahau wasanii wa kweli, siyo tu unaharibu sanaa ila kuwatukana wasanii.

Mtu wa hadhi na vituko vya Amber Lulu anatoa ujumbe gani kwa jamii, kupitia maisha yake? Kama Amber Lulu anadiriki kusema hadharani ili dunia nzima imsikie kuwa yeye cha muhimu kwa mwanaume ni pesa.

Kwamba yuko tayari kuwa na yeyote na kufanya lolote naye kama tu huyo anaweza kuutunza mwili wake na kumpa mkwanja.

 Huyu mtu anawafunza nini wasichana wenye miaka kuanzia kumi na nne na kuendelea?  Ninachoweza kusema ni kwamba, Amber Lulu na wenzake na namna hiyo wamevamia Bongo Fleva japo hawawezi kuivunja kama mamisi walivyofanikiwa katika Bongo Muvi.

Misingi na mizizi ya Bongo Fleva ni migumu sana.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles