31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEISHI NA MKASI TUMBONI MIAKA 18 VIETNAM AFANYIWA UPASUAJI

mkasiMadaktari nchini Vietnam wametoa mkasi wa kufanyia upasuaji kutoka kwenye tumbo la mwanamume mmoja baada ya kukaa na mkasi huo kwa miaka 18.

Wataalamu wa upasuaji walisafiri kwa ndege kutoka mji mkuu wa Hanoi kusaidia katika upasuaji huo uliofanyika katika mkoa wa Thai Nguyen kaskazini mwa nchi hiyo.

Mgonjwa huyo wa umri wa miaka 54 alifika hospitalini baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani mwezi jana.

Lakini baada yake kupigwa picha ikagunduliwa kwamba alikuwa na kifaa cha chuma chenye ncha kali sehemu ya kushoto tumboni.

Alipimwa tena katika hospitali iliyo karibu katika mkoa jirani wa Bac Kan na ikabainika bila shaka kwamba alikuwa na mkasi wa urefu wa sentimita 15 (inchi 6) karibu na utumbo wake mkubwa, gazeti la Tuoi linasema.

Ma Van Nhat anasema huenda mkasi huo uliachwa mwilini mwake alipofanyiwa upasuaji katika hospitali kuu ya mkoa wa Bac Kan mwaka 1998 baada yake kuhusika katika ajali nyingine ya barabarani, kwa mujibu wa gazeti la Vietnam Express. Source BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles