23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Al shabaab waua polisi watano Kenya

 Joseph Boinnet
Joseph Boinnet

NAIROBI, KENYA

MAOFISA watano wa polisi wameuawa baada ya mshukiwa wa ugaidi kumpokonya askari bunduki na kuwafyatulia risasi.

Mshukiwa huyo alikuwa amefungiwa korokoroni baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga na mtandao wa kigaidi wa Al Shabaab.

Alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kapenguria, Kaskazini Magharibi mwa Kenya.

Awali iliripotiwa kuwa mtu huyo alivamia kituo hicho ili kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi.

Mkuu wa Polisi wa kituo hicho, Vitalis Ochido, ambaye awali alitangazwa kujeruhiwa, naye amefariki dunia kutokana na majeraha.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinnet, alisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.

“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anashikiliwa, alitwaa bunduki na kuanza kufyatua risasi,” Boinnet amenukuliwa akisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles