Aga Khani yajivunia matibabu ya nyuklia

0
878

Tunu Nassor _Dar es Salaam 

Hospitali ya Aga Khan (AKHD) imeadhimisha wiki ya matibabu ya nyuklia huku ikijivunia kuwa na teknolojia ya kisasa ya kupima magonjwa mbalimbali kupitia mashine ya ‘Spect Gamma camera’.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Oktoba 5, Mkurugenzi wa Tiba wa hospitali hiyo, Dk. Ahmed Jusabani amesema kuwapo kwa teknolojia hiyo hospitalini hapo kumerahisisha kugundua magonjwa yakiwa katika hatua za mwanzo.

Amesema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kugundua magonjwa mbalimbali yakiwamo ya watoto, ya ubongo, figo, mifupa, saratani, tezi na mifupa.

“Tiba hii inatumia kiwango kidogo cha mionzi ukilinganisha na ile ya X-rays hivyo kupunguza athari zitokanazo na mionzi hiyo kuingia mwilini,” amesema Jusabani. 

Naye Daktari Bingwa wa Radiolojia kutoka Taasisi ya saratani ya Ocean Roads (ORCI ), Dk Tausi Maftah amesema matibabu ya nyuklia hutibu saratani ya Goita na kupona kabisa.

“Mashine hii husaidia kuchunguza moyo uliosimama kama umekufa ama unaweza kuamshwa na ukaendelea kufanyakazi,” amesema Dk.Tausi.

Hata hivyo amesema changamoto iliyopo ni mashine hizo kuwa chache nchini kwa kuwa zinapatikana katika hosptali za AKHD, ORCI na Bugando Mwanza jambo ambalo linawalazimu wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here