28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Ado ajitosa ukatibu mkuu ACT Wazalendo

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KIVUMBI cha Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama cha ACT Wazalendo sasa kimepamba moto, baada ya Katibu wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma ya chama hicho, Ado Shaibu kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu.

Hatua hiyo sasa inafanya idadi ya wanachama waliojitokeza kuwania ukatibu mkuu kufikia watatu. Wengine ni Kaimu Katibu Mkuu wa sasa, Doroth Semu na Joran Bashange.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu, Shaibu alisema kuwa baada ya tafakuri ya kina, kufanya tathmini ya kisayansi na kwa kuzingatia masilahi mapana ya chama chake, ameamua kuchukua fomu kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo.

Alisema nafasi hiyo inawaniwa tofauti na vyama vingine vya siasa ikiwamo CCM, ambavyo Katibu Mkuu uteuliwa.

“Ukatibu Mkuu wa ACT Wazalendo ni wa kugombea. Kabla ya mtu kuwa Katibu Mkuu ni lazima kwanza agombee na kuchaguliwa na Halmashauri Kuu ya chama. 

“Binafsi nimefarijika kuona tayari wanachama wawili, Ndugu Dorothy Semu na Joran Bashange wamechukua fomu za kuwania nafasi hii. 

“Wote wawili ninawafahamu vyema na ni watu ninaowaheshimu. Nina imani sisi watatu, iwapo tutateuliwa kuwa wagombea, tutaipa Halmashauri Kuu fursa ya kipekee ya kuchagua Katibu Mkuu bora anayeendana na wakati tunaoishi,” alisema Shaibu.

Alisema hivi sasa vyama vya upinzani vinapitia kwenye kipindi cha kipekee ambacho kinahitaji Katibu Mkuu wa kipekee pia.

“Tunaishi katika zama ambazo CCM na Serikali yake inawahofia viongozi wetu wakuu kupita kiasi na wamepanga njama mara kadhaa kuwafungia kisiasa, kufuta chama, kuwabambikia kesi zisizo na dhamana. Tunamuhitaji Katibu Mkuu atakayeielewa hali hii vizuri na atakayekilinda chama chetu kwa wivu mkubwa,” alisema Shaibu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles