22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

ADAIWA KUFANYA SHAMBULIO LA AIBU KWA MTOTO

MANENO SELANYIKA NA DORIS KESSY (TSJ)

MKAZI wa Kiluvya  Dar es Salaam Paul Augustino (30), amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akituhumiwa  kufanya shambulio la aibu dhidi ya mtoto (jina tunalo) mwenye umri wa miaka sita.

Mwendesha mashtaka, Daisy Makakala alidai mbele ya Hakimu, Joyce Moshi  kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 22, mwaka jana huko Kiluvya  Kwa Komba wilayani Ubungo.

“Unadaiwa ulimuingiza vidole mtoto huyo sehemu zake za siri kisha kumdhalilisha kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Daisy.

Mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai   upelelezi   haujakamilika.

Hakimu Joyce alisema  shtaka hilo kwa majibu wa sheria linadhaminika hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua kutoka Serikalini ama taasisi inayojulikana katika sheria.

Mtuhumiwa alirudishwa mahabusu hadi Machi 13, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles