ADADI AWAFUNDA WABUNGE JINSI YA KUVAA, KULA

0
748

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu amesema wabunge wana wajibu wa kuangalia mavazi yao na jinsi ya kula mbele za watu.

Adadi amesema hayo leo wakati akichangia katika semina ya wabunge wa Kamati za Bunge kuhusiana na masuala ya Kidiplomasia na Itifaki, iliyoandaliwa na Bunge kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wabunge na wawakilishi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP).

Amesema wabunge wana wajibu wa kuangalia ni wakati gani na namna gani wanatakiwa kuvaa nini ili kuendana na mazingira ya eneo husika.

“Tuna wajibu wa kujiangalia jinsi tunavyokula tukiwa mbele ya macho ya wengi, siyo unajaza tu chakula mdomoni, hili la mavazi pia ni lazima tuliangalie kwani katika mavazi yetu unakuta Rais kavaa tai nyekundu na wewe unavaa tai nyekundu hapana, anayetakiwa kuvaa tai nyekundu ni Rais tu,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here