23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ACT kushirikiana na vyama vya upinzani kutetea demokrasia

Mwandishi wetu , dare s salaam

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimepanga kuimarisha ushirikiano kati yao na vyama vingine vya upinzani nchini katika kuipigania, kuitetea na kuilinda misingi ya kidemokrasia ambayo imevurugwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano.

Hayo yameelezwa leo na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe alipokuwa akiwasilisha maazimio ya kamati hiyo leo Juni katika ofisi ndogo ya chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa wamepanga kujaduku namna namna vya upinzani vitakavyoshirikiana katika uchaguzi ujao.

“Kamati Kuu imewaagiza viongozi wakuu wakuu wa chama kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye ushirikiano na vyama vingine na pia kuhakikisha utekelezaji thabiti wa Azimio la Zanzibar lililoutangaza mwaka huu kuwa mwaka wa mapambano ya kudai demokrasia” amesema.

“Pia, Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu wa Chama kuwaandikia makatibu wakuu wa vyama vyote tunavyoshirikiana navyo kuitisha kikao cha viongozi wakuu kutafakari namna bora ya vyama vya upinzani kushirikiana kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles