25.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

ACB yazindua kadi ya Visa kukidhi matarajio ya wateja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya Akiba (ACB) imezindua huduma ya kadi za VISA ambazo ni mahususi kwa kufanya miamala ya kifedha na ina uwezo wa kutumika sehemu yoyote duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, Silvest Arumasi, amesema benki inafanya maboresho makubwa ya huduma za kifedha kwa wateja wake ili kuendana na mahitaji ya soko.

Amesema maboresho hayo yatasaidia kukidhi matarajio ya wateja ambapo hivi sasa huduma nyingi za kibenki zinatolewa kidigitali na kusaidia kupata huduma kwa haraka na rahisi zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba (ACB), Silvest Arumasi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi za VISA.

“Huduma za ACB VISA CARD zinamrahisishia mteja kufanya miamala mbalimbali kidigitali mfano; kutoa pesa kwenye ATM mbalimbali za VISA popote duniani na kufanya manunuzi mtandaoni, kufanya malipo kwenye vituo vya mafuta, kwenye migahawa na kwenye maduka makubwa na nyingine nyingi,” amesema Silvest.

Amewashukuru wateja wa benki hiyo kwa kuendelea kuiamini na kufanya biashara na kuwaomba wajasiriamali na wafanyakazi kutoka taasisi za umma na binafsi kujiunga na ACB ili kufurahia huduma bora zaidi kwa haraka, unafuu na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles