27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi watatu wafariki dunia kwa kugongwa na gari wakitoka shuleni Arusha

JANETH MUSHI -ARUSHA

WANAFUNZI watatu wa Shule ya Sekondari Olmoti iliyopo Mkoa wa Arusha, wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati wakitoka shule huku wengine wawili wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni, tukio hilo lilitokea Agosti 6 mwaka huu, majira ya saa 11:30 jioni katika barabara ya Afrika Mashariki, Wilaya ya Arusha.

Kamanda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Christina Mkondola, (16) mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Rebeca Msengi (16)  kidato cha pili na Ben Naiman (15) mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wote walipotezea maisha eneo la tukio.

Kamanda Hamduni aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Elevira Epodi (16) na Shamira Nkini (14) wa kidato cha kwanza ambao wanaendelea kupatiwa matibabu na katika Hospitali ya Rufaa Mount Meru.

Alisema siku ya tukio gari lenye namba T.768 BKL aina ya JEEP lililokuwa likiendeshwa na Sariko Mwenda (64) liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao waliokuwa wakitembea kwa miguu pembezoni mwa barabara hiyo.

Alidai uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva huyo kuendesha gari kwa mwendo kasi na kujaribu kuyapita magari mengine yaliokuwa mbele yake na kushindwa kulimudu gari hilo.

 “Baada ya dereva huyo kupoteza uelekeo aligonga gari lililokuwa ubavuni mwake lenye namba za usajili T.251 AJB aina ya Touota Hilux Double Cabin na baiskeli moja na ajali hiyo imetokea wakati gari hilo likitokea  Usa river kuelekea mzunguko wa Kisongo,”alisema

“Dereva huyo liwagonga watembea kwa miguu hao  ambao wote ni wanafunzi wa shule hiyo na walikuwa upande wa kushoto wa barabara  wakitokea shuleni kuelekea nyumbani  kwao,”alisema.

Kamanda Hamduni alisema mtuhumiwa huyo  amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

Alitoa wito kwa madereva kuchukua tahadhali pindi wanapotumia vyombo vya moto na kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za usalama wa barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles