26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC Simiyu: Hoteli hazitatumika kuhifadhi wagonjwa wa corona

Derick Milton, Busega

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amesema mkoa huo hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona badala yake watatumia shule za sekondari za bweni.

Amesema wameamua kuchukua uamuzi huo ili kuwapunguzia wagonjwa hao gharama za kuishi katika siku zote ambazo watakuwa karantini na kwamba utaratibu huo hautawafunga watu wenye uwezo ambao watapenda kwenda hotelini.

Mtaka ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 31, alipokuwa akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa shule ya sekondari Mtaka iliyopo Wilayani Busega kutoka kwa Viongozi wa Umoja wa Makanisa 21 ya Kikristo Tanzania kata ya Lamadi.

Amesema tayari kila Wilaya imetenga shule yenye vitanda vya kutosha na mazingira mazuri kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa huo, huku akiwataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari.

“Kama mkoa tumeamua kuwa hatutatumia hoteli kuhifadhi mtu yeyote ambaye atabainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, tumeamua kuwa tutatumia shule za sekondari za bweni labda mtu mwenyewe aamue kupelekwa katika hoteli ambazo na zenyewe tumeziainisha,” amesema Mtaka.

Katika hatua nyingine amewataka wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mitihani mkoani humo kuhakikisha wanawasimamia watoto wao kuhakikisha wanajisomea katika wa kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles