Aliyekuwa Katibu Mkuu CUF kuzikwa Dar leo

0
868

Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleyman Khalifa anatarajiwa kuzikwa leo Jumanne Machi 31, katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Khalifa alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akitibiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya ini.

“Kwa hakika chama kimepata pigo kubwa na kwa yakini marehemu ameacha pengo ambalo haliwezi kuzibika kirahisi,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here