28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA MAUMIVU MWANZA

ASHA KIGUNDULA-MWANZA

WAWAKILISHI  wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Yanga,  imejiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu hatua ya makundi, baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 2-1,  kutoka kwa Pyramids ya Misri, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Timu hizo zitarudiana Novemba 3, katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa June 30, Cairo nchini Misri.

Matokeo ya jana yana maana kwamba, Yanga itatakiwa kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 na kuendelea ili kufuzu hatua ya makundi.

Mchezo huo ulianza taratibu lakini kadri muda ulivyozidi kusonga ndivyo kasi ilivyoongezeka, huku yakishuhudiwa mashambulizi ya kupokezana.

Baada ya kosakosa  za kila upande, dakika ya 42 Eric Traore aliiandikia Pyramids bao la kuongoza, baada ya kuunganisha krosi ya Mohamed Farouk.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipokamilika. Kipindi cha pili , Pyramids  mkakati wa Pyramids ulizaa matunda dakika ya 62, baada ya kiungo mkongwe  Mohamed Fathy kuifungia bao la pili.

Hata hivyo, Yanga haikukata tama licha ya kutanguliwa kwa mabao hayo mawili.

Dakika ya  88, Papy Tshishimbi aliifungia Yanga  kwa mkwaju wa mguu wa kushoto uliomshinda kipa wa Pyramids , Ahmed Elshanawy.

Yanga ilipata pigo dakika ya pili ya nyongeza, baada ya zile 90 za kawaida kukamilika, ambapo beki wa timu hiyo Kelvin Yondan alilimwa kadi  ya pili ya njano kabla ya kuonyeshwa nyekundu iliyomlazimisha kutoka nje.

Hadi kipyenga cha kuashirikia kumalizika kwa pambano hilo kinasikika, Pyramids ilitoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo, pia wachezaji Mrisho Ngassa, Tshishimbi, Abdulazizi Makame walionyeshwa kadi za njano, huku Johe Atwi, Ahmed Mansour wakilimwa kadi za njano kwa uoande wa Pyramids.

Katika tukio jingine lililotokea baada ya mchezo huo kumalizika, mashabiki wa Yanga walisikika walipaza sauzi wakiutaka uongozi wa klabu yao umfungashie virago Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

Yanga iliangukia Kombe la Shirikisho, baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na Zesco United  ya Zambia,  kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2. 

Pyramids kwa upande wake, iliiondosha mashindanoni Etoile Du Congo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, zilipokutana raundi ya awali kabla ya kutinga raundi ya kwanza na kuitimua CR Belouizdad ya Algeria kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

Mara ya mwisho Yanga kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika  ilikuwa mwaka 2017,  baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya Wolayta Dichaa ya Ethiopia.

Pyramids inashiriki michuano hiyo kwa mara kwanza. Ilikata tiketi hiyo  baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Misri,   nyuma ya mabingwa Al Alhly na Zamalek iliyomaliza nafasi ya pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles