33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga, Azam, Simba vitani

Pg 32 Okt 17NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

LIGI Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi sita katika viwanja tofauti huku Yanga ikiikaribisha Azam FC katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga, Azam na Simba zitakuwa zikicheza kusaka ushindi katika mechi zao ili zijiweke katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ina pointi 15 sawa na Azam lakini inaongoza kwa kupachika mabao 13 huku Azam ikiwa na mabao 9, hivyo kila moja itakuwa ikisaka ushindi ili kuongoza ligi hiyo.

Wakati Yanga na Azam zikiwania usukani wa ligi hiyo, Simba wao watakuwa katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuvaana na wenyeji Mbeya City.

Simba ambayo inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 12, itakuwa ikisaka ushindi ili kufuta uteja kwa Mbeya City, kutokana na kufungwa kila inapocheza katika uwanja huo.

Yanga na Azam zina rekodi nzuri tangu kuanza kwa ligi hiyo, kwani zote hazijawahi kupoteza mchezo hata mmoja katika mechi zake hadi sasa.

Yanga wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, wakaifunga Tanzania Prisons mabao 3-1, wakaifunga JKT Ruvu mabao 4-0, mechi zote zikichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kufuta uteja kwa Mtibwa Sugar, kwa kuifunga mabao 2-0, katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Azam wao wameifunga Coastal Union mabao 2-0, wakaifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, wakainyuka Stand United mabao 2-0, wakaichapa Mwadui bao 1-0, kisha kuinyuka Mbeya City mabao 2-1 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Simba katika kujihakikishia wanafanya vizuri kwenye mchezo huo, walitinga mapema mkoani Mbeya kuanza mazoezi, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, amejihakikishia ushindi licha ya kutambua kuwa mchezo utakuwa mgumu.

Katika michezo mingine ya ligi hiyo,  Majimaji itaikaribisha African Sports katika Uwanja wa Majimaji, mkoani Ruvuma huku Ndanda FC ikiwaalika Toto African katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Coastal Union itaikaribisha Mtibwa Sugar na Stand United itaikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles