29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

UN: Demokrasia ya dunia imetekwa nyara

UN, NEW YORK

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameionya dunia juu ya kuonyeshana ubabe na kutekwa nyara kwa demokrasia huku makundi ya kizalendo yakiongezeka.

Akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza Kuu la UN mjini hapa juzi, Guterres alisema dunia inakabiliwa na hali mbaya ya kukosekana hali ya kuaminiana huku demokrasia ikihujumiwa.

Akihutubia viongozi kutoka nchi 133 duniani, Guterres aliutolea mwito ulimwengu kurudisha imani katika suala zima la kuaminiana wakati huu, ambao dunia inakabiliwa na matatizo chungu nzima kuanzia mabadiliko ya tabia nchi hadi ugaidi na migogoro.

Guterres amewaonya viongozi kuwa kanuni za dunia zinazidi kuvurugika wakati imani ikiwa katika kilele cha kuporomoka huku mabadiliko madarakani yakitishia kuzuka kwa vita.

”Dunia yetu inakabiliwa na hali nyingi za ukosefu wa kuaminiana, watu wana mashaka na hofu. Na hali ya uaminifu imefikia ukingoni. Iwe ni uaminifu kwenye taasisi za kitaifa, miongoni mwa mataifa na katika sheria za kimataifa.”

“Ndani ya nchi watu wanapoteza imani na mifumo ya kisiasa. Uimla umeongezeka na makundi ya siasa kali za kizalendo nayo yanaibuka,” amesema.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa UN hakumlaumu yoyote moja kwa moja katika hutuba yake hiyo, ambayo inakuja huku kukiwa na hali ya mvutano kati ya Marekani na Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles