28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI KUNUFAIKA NA MIKOPO

                                                                 |Susan Uhinga, Tanga


Vijana wametakiwa kujiunga kwenye vikundi, ili Serikali kupitia Halmashauri iwawezeshe katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa na Ofisa Vijana wa Jiji la Tanga, Omari Ally akizungumza Mtazania Digital, kuhusu uwezeshwaji kwa vijana jijini humo.

Amesema kumekuwa na changamoto kwa vijana namna ya kujiunga katika vikundi kutokana na sababu mbalimbali lakini pia kitengo cha vijana kimeweza kutoa elimu kwa vikundi vipatavyo 25 kwenye kata 10 za Halmashauri ya jiji la Tanga ambavyo vitanufaika na mikopo.

“Vijana wajiunge kwenye vikundi kwani serikali kupitia kitengo cha vijana imetenga Fedha kwa ajili ya kuwawezesha ili waweze kujikwamua na umasikini,” amesema.

Akizungumzia changamoto ya vikundi vingi kufa mara baada ya kupata mkopo Ofisa Vijana huyo amesema wanaitambua changamoto hiyo na kwa sasa inafanyiwa kazi hasa kwa kuhakikisha wanajikita zaidi kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo na namna ya kujiendesha.

“Kwa sasa tatizo la vikundi vya vijana kuparanganyika limepungua kwa kuwa Elimu inawafikia na wanaelewa, tunavyo vikundi vya mfano wameweza kufanya vizuri hasa kikundi cha vijana wa Pongwe,” amesema Omari.

Mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles