29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

R. KELLY: HESHIMA YANGU IMEPOTEA

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Robert Kelly maarufu kwa jina la R. Kelly, amekubali kuwa unyanyasaji wa kijinsia umemfanya apoteze heshima yake kwa mashabiki.

Amedai kwamba amekuwa katika kipindi kigumu tangu atuhumiwe kuwanyanyasa kijinsia wasichana, hivyo atahakikisha anaandaa wimbo kwa ajili ya kulielezea hilo.

“Sikutegemea kama hali ingekuwa hivi, kwa sasa nimekuwa msanii ambaye siheshimiki kwa mashabiki, ninatarajia kuandika wimbo ambao utaelezea mambo yote niliyoyapitia, ninaamini ujumbe huo utawafikia watu na kuufanyia kazi.

“Ninajitupia lawama kwa kila nilichokifanya, sasa nataka kuwa mwaminifu kwa mashabiki zangu,” alisema R. Kelly.

Msanii huyo alikumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wasichana wadogo kwa kuwalazimisha tangu mwaka 2008.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles