22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

MAUA SAMA: HAIKUWA KAZI RAHISI KUKAMILISHA AMEN

Na JENNIFER ULLEMBO – DAR ES SALAAM


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Maua Sama, amefunguka na kusema kuwa haikuwa kazi rahisi kuandaa video ya wimbo wake mpya wa Amen.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Maua alisema ilimchukua takribani saa kadhaa kutengeneza kila kipande kilichopo ndani ya wimbo huo mpya aliomshirikisha Bernad Paul ‘Ben Paul’.

“Kufanya video si kazi rahisi kama wenzetu wanavyofikiria, ukweli nimepata tabu sana katika video yangu ya Amen, kuna baadhi ya vitu vilikuwa ni vigumu kuvifanya kwa harakaharaka,” alisema Maua.

Alisema ana imani wimbo na video ya Amen utapokelewa vema na mashabiki wake ambao wamekuwa wakitamani kumuona akifanya kazi nzuri zaidi zitakazoweza kumsaidia kukuza muziki wake.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles