27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

UWOYA, HAMISA WANUSA JELA

Na JOHANES RESPICHIUS


HIVI karibuni Mwigizaji, Irene Uwoya na Mwanamitindo, Hamisa Mobetto kidogo waende jela miaka saba au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kuchapicha picha za utupu.

Hivyo kwa huruma ya Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliwaamuru wasanii hao kuombe radhi kwa kuchapisha picha za utupu mitandaoni na iliwapa onyo kama wakirudia watalazimika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kutokana na hatua hiyo SWAGGAZ wiki hii imeona ni vyema kukuletea baadhi ya vifungu vya sheria hiyo ambavyo endapo wasanii hao wakirudia kufanya kosa hilo au mtu mwingine akichapisha video au picha za utupu anaweza kuhukumiwa navyo.

ISEMAVYO SHERIA

Sheria hiyo ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015 inawahusisha watumiaji wa mitandao kama Facebook, WhatsApp, Instagram, Twitter, barua pepe (emails), blogu na nyinginezo.

Katika sheria hiyo kifungu cha 14 (1) inasema kuwa mtu hawezi kuchapisha au kusababisha kuchapishwa kupitia mfumo wa kompyuta au njia nyingine yoyote ya teknolojia ya habari na mawasiliano kusambaza picha au video za ngono ama zinazoashiria vitendo vya ngono.

Kifungu cha 14 (2)kinasema mtu atakayekwenda kunyume na kifungu cha kwanza nafanya kosa na anaweza kuhukumiwa kwa kukutwa na hatia kwa kosa la kuchapisha picha au video za ngono.Mtu atakayefanya kosa hilo faini yake sio chini ya Sh milion 20 au kifungo cha muda usio usiopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.

TCRA

Wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati, Valerie Msoka, alisema Uwoya na Mobetto wanatakiwa kuomba radhi kutokana na kukiuka kanuni za maudhui mtandaoni 2018 kwa kuchapisha picha za utupu mtandaoni.

Kosa la Hamisa alilitenda Aprili 10 na Juni 23, mwaka huu kwa kuchapisha picha kwenye mtandao wa Instagram zikimwonyesha mjamzito huku akishikwa juu ya tumbo karibia sehemu za siri jambo linaloweza kusababisha watoto kuiga tabia mbaya.

Msoka alisema Mobetto alikiri kusambaza na kudai alizipiga akiwa nchini Kenya kwa malipo mwaka jana kabla ya sheri ya mtandao kupitishwa kwamba hakuchapisha kwenye kurasa zake hivyo ni vigumu kuwataka watu wengine wazifute.

“Hamisa anapewa onyo, endapo atatenda tena kosa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake, pili, aombe radhi na kuwaelimisha mashabiki zake juu ya matumizi ya picha zisizo na maadili,” alisema Msoka.

Alisema Uwoya alichapisha picha zinazoonyesha maungo ya mwili wake kitendo ambacho ni kinyume cha maadili ya Tanznaia Juni 26, mwaka huu.

Alisema baada ya kuhojiwa Uwoya naye alikiri kutenda kosa na kuomba radhi na kwamba alifanya hivyo kwa kumuiga ‘role model’ wake Beyonce.

WALIVYOOMBA RADHI

Muda mfupi baada ya agizo la TCRA wasanii hao kila mmoja akitumia mtandao wake wa Instagram waliomba radhi kwa watanzania kwa kuchapicha picha hizo ambazo zinakiuka maadaili ya mtanzania.

UWOYA

Mwigizaji wa filamu za kibongo, Irene Uwoya aliandika; “Wapenzi wangu, ndugu zangu,  wakubwa zangu na wadogo zangu naomba radhi kwa picha niliyoposti… najua niliwakwaza mnisamehe sana sikujua ntawakwaza ni sababu tu ya ‘role model’ wangu Beyonce, nimejifunza sasa… nawapenda.

HAMISA

Mwanamitindo Hamisa Mobetto aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuomba radhi kwa kitendo cha yeye na mashabiki zake kuchapisha picha ambazo zinamwonyesha nusu utupu na kuwataka wasirudie kufanya hivyo.

“Naomba kutumia fursa hii kuomba radhi kwa watanzania na wote wanaotumia mitandao kwa kitendo cha mimi na washabiki zangu kutuma picha zangu zinazoonyesha nusu utupu kwenye kurasa zao za Instagram.

“Niwahusie vijana wenzangu kuepuka kutumia vibaya mitandao ya kijamii kuna sheria kali zinazokataza kutuma picha mbaya mitandaoni, pia nawaomba mashabiki zangu kuanzia sasa kutumia picha zangu zenye staha au kutumia biashara zangu kunisapoti,” aliandika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles