28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Chenge azua mtafaruku

ChengeNa Samwel Mwanga, Simiyu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshutumu Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) kuwa alitumia bastola yake kupiga risasi juu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliokuwa katika ofisi za chama mkoani Simiyu na kuzua taharuki kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi jana, aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana (BAVICHA), John Heche alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 eneo la Salunda.
Hata hivyo, madai ya Chadema yametofautiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi baada ya kueleza kuwa aliyefyatua risasi hakuwa Chenge, bali ni mmoja wa watu waliokuwa katika gari la mbunge huyo, Ahmed Ismail.
Alisema uchunguzi wa awali,umebaini Ismail alilazimika kutumia bastola hiyo ili kujihami kutokana na kundi la watu waliokuwapo eneo hilo kuanza kuwashambulia kwa mawe.
“Katika tukio hili hakuna mtu aliyejeruhiwa,Polisi tunaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli, tunashukuru hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kwa risasi,” alisema.
Awali akielezea tukio hilo, Heche alisema baada ya kumaliza mkutano wa chama hicho uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu-Bara, John Mnyika waliamua kutembea miguu kuelekea kwenye ofisi za chama chao.
Alisema baada ya kufika ofisini, walifanya kikao cha ndani, ghafla magari matano ambayo yanasadikiwa yalikuwa kwenye msafara wa Chenge yalisimama kwenye ofisi zao.
Katika magari hayo, moja wapo lilikuwa na sipika kubwa za simu, huku Chenge akishuka na kucheza muziki mbele yao.
Kutokana na hali hiyo, mmoja wa walinzi wa Chadema aliwaomba waondoke eneo hilo, lakini wakakaidi.
Alisema muda mfupi wafuasi wa Chadema walifika na kuyazingira magari, ndipo Chenge alipoingia ndani ya gari na kuchukua bastora.
“Hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa mpaka mkutano wetu ukavunjika..tuliamua kwenda polisi na kufungua faili lenye namba BAR/RB/1195/2015.
Chenge alipotafutwa jana kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.
Lakini alipotumiwa ujumbe mfupi (sms), alijibu kupitia kwa mmoja wa wasaidizi wake kuwa suala hilo liko polisi hawezi kulizungumzia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles