33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mgodi wa Buzwagi kufungwa

Na Fredrick Katulanda, Mwanza

MAKAMU wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika, amesema mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga utafungwa kutokana na uzalishaji kushuka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanyika alisema mashapo ya dhahabu ya mgodi wa Buzwagi yana uwezo wa kutoa Ounce 900,000 ya dhahabu yenye ubora wa gramu 1.35 kwa tani hivyo kudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Alisema kutoka na hali hiyo, uongozi wa Kampuni ya Acacia utalazimika kuufunga mgodi huo na kuelekeza nguvu kwenye migodi ya Bulyankhulu na North Mara.
Alisema upande wa mgodi wa North Mara uliopo Wilaya ya Tarime, unao uwezo wa kutoa Ounce milioni 2.02 ambazo zina ubora wa gramu 2.6 kwa tani moja.
Alisema mgodi wa Bulyankhulu una kiasi kikubwa cha mashapo yenye uwezo wa kutoa Ounce milioni 9.2 ambazo zina ubora wa gramu 9.7 kwa tani moja hivyo kukadiriwa kuwa na muda mrefu wa kuendelea na uzalishaji kwa miaka 40 hadi 60 ijayo.
Alisema kutokana na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dhahabu duniani, migodi yote ya Acacia imeanza kujielekeza kupunguza gharama za uzalishaji.
Katika hatua nyingine, alisema Kampuni ya Acacia imefanikiwa kulipa Sh bilioni 2.2 za ushuru wa huduma kwa halmashauri za wilaya ya Tarime mkoani Mara, Msalala na Kahama mkoani Shinyanga kuanzia Juni hadi Desemba, mwaka jana.
“Tulilipa ushuru wa huduma Sh milioni 863 (Tarime), Sh milioni 749 (Msalala) na Sh milioni 843 kwa Halamshauri ya Wilaya ya Kahama. Changamoto kubwa na namna ambayo fedha hizo zitatumika huko ili wananchi waone faida ya uwapo wa migodi nadhani hili linapaswa kufuatiliwa zaidi,” alisema.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles