29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

WB YAONYA UKOPAJI HOLELA UNAOZIDISHA DENI LA TAIFA

Na Mwandishi Wetu,

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Makhtar Diop, ameionya Serikali dhidi ya ukopaji  holela na kufanya ongezeko la deni la taifa  kuwa asilimia tatu ingawa deni  hilo bado himilivu kwa uchumi wa taifa.

Diop aliyasema hayo wiki mbili zilizopita baada ya kufanya  mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alipotembelea wizara hiyo.

“Serikali inatakiwa kuwa makini katika ukopaji holela ili deni la taifa libakie kuwa endelevu,” alisema Diop.

Kuwekuwapo na wasiwasi kuhusu ongezeka kwa deni la taifa ambalo linaweza kuwa mzigo kwa wananchi hasa wa  hali  ya chini.

Katika ripoti ya benki iliyotolewa na Benki Kuu wiki iliyopita, inaonyesha kuwa deni la nje la taifa kufikia mwishoni mwa Novemba mwaka jana, lilifikia Dola za Marekani milioni 16.528.6 (debt stock) ambalo ni ongezeko la Dola milioni 121 ikilinganishwa na mwezi uliotangulia.

Katika kila mwaka, madeni yalikuwa dola milioni 802.7 kuliko kiasi (disbursements) kilichotolewa Novemba mwaka jana cha jumla dola milioni 121,5, ambapo dola milioni 101.2 ilipokelewa na Serikali Kuu na kiasi cha fedha kilichobaki cha dola milioni 20.3 ilikuwa sekta binafsi.

Kila mwaka kiasi cha fedha kinachotolewa ni jumla ya dola milioni 1.423.3 milioni huku dola milioni 914.6 ilikuwa kwa ajili ya Serikali Kuu.

Katika deni la nje, kiasi cha dola milioni 35.4  kililipwa Novemba mwaka jana, ambapo  Serikali Kuu ilikuwa imelipa dola milioni 28.2 na iliyobaki ililipwa na sekta binafsi.

Kwa mwaka unaoishia Novemba 2016, deni la huduma, jumla ya dola milioni 1.022.4  ambayo kiasi cha dola milioni 710.7 zililipwa na Serikali na iliyobakia na sekta binafsi. Kwa upande wa deni la ndani, ilikuwa Sh bilioni 10.166.8 mwishoni mwa Novemba mwaka jana ambalo ni ongezeko la Sh bilioni 77.5.

Mabenki ya kibiashara bado yanaongoza katika uwekezaji wa deni la ndani.

Aidha, deni jipya lililotolewa kwa ajili ya bajeti ya Serikali kwa ajili ya Novemba mwaka jana, ilifikia Sh bilioni 488.8, huku Sh bilioni 150.3 ilikuwa (Treasury bonds) na Sh bilioni 338.5  ilikuwa (Treasury bills).

 Aidha, hotuba ya Waziri wa Fedha bungeni wiki iliyopita, ilisema deni la taifa hadi kufikia Desemba mwaka jana  kwa ujumla wake lilifikia Dola za Marekani milioni 19,021.9 (debt stock) ikilinganishwa na dola milioni 18,459.3 Juni mwaka jana, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 3.05.

Kiasi hiki cha deni hakijumuishi deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii linalokadiriwa kufikia dola milioni 1,725.8, ingawaje deni hilo limezingatiwa katika tathmini ya uhimilivu wa deni la Taifa.

Ongezeko la deni hilo limetokana  na mikopo iliyopo na mipya iliyopokelewa na Serikali na ambayo bado haijaiva kutoka mikopo ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ulipaji wake, Serikali imekuwa ikilipa madeni ya nje na ndani kuanzia Julai mwaka jana na hadi kufikia Desemba mwaka jana, Serikali ilitumia jumla ya Sh bilioni 2,570.1 kulipia madeni ya ndani na nje yaliyoiva.

Kati ya kiasi hicho, malipo ya deni la ndani ni Sh bilioni 1,822.3 na deni la nje ni Sh bilioni 747.8.

Malipo ya deni la ndani yanajumuisha malipo ya mtaji (rollover) ya Sh bilioni 1,367.1 na malipo ya riba ya Sh bilioni 455.2

Katika upande wa tathmini ya Uhimilivu wa Deni la Taifa, anasema kwa tathmini hiyo inaonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu. Matokeo hayo yanafanana na yale yaliyotolewa katika taarifa ya IMF ya uhimilivu wa deni la taifa iliyotolewa Juni mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles