26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YASHINDA UMEYA KIGAMBONI

ccm

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam baada ya mgombea wake, Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi, Maabadi Hoja, kupata kura tisa kati ya 15 zilizopigwa na wajumbe katika uchaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni.

Hoja alipata ushindi huo akimbwaga Celestine Maufi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyepata kura tano.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Halmashauri hiyo, Rahel Mhando, alisema kati ya kura 15 zilizopigwa moja iliharibika.

“Maabadi Hoja kapata kura tisa kati ya 15 zilizopigwa, mshindi wa nafasi ya Naibu Meya ni Amin Sambo wa CCM aliyepata kura 10 akifuatiwa na Ernest Mafimbo wa CUF aliyepata kura tano,” alisema Mhando.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba, aliwataka wajumbe kufanya kazi kwa kuwa chombo cha kutoa uamuzi kimeshapatikana.

Hoja aliwahi kuwa Meya wa Manispaa ya Temeke katika kipindi cha mwaka 2010-2015 na mwaka huu kabla ya kugawanywa kwa manispaa hiyo, alijipanga kugombea tena kiti na kushindwa na Abdallah Chaurembo.

Ushindi wa Hoja umewezesha CCM kuongoza halmashauri tatu jijini Dar es Salaam ambazo ni Kigamboni, Kinondoni na Temeke wakati vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiongoza halmashauri mbili za Ubungo na Ilala na Jiji la Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles