32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE YAVAMIWA BAADA YA JIJI KUSHINDWA KULIPA FIDIA

shule-ya-msingi

Na BENJAMIN MASESE, MWANZA

ENEO la Shule ya Msingi Kanindo, iliyopo Kata ya Kishili, limevamiwa na wakazi ambao wamejenga nyumba huku waking’oa vigingi  vya mipaka vilivyowekwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza mwaka 2012.

Uvamizi wa eneo hilo umeonekana kuanza  kufuta ndoto za mpango uliopo wa kujengwa shule ya sekondari ili kuondoa usumbufu wa wanafunzi maeneo hayo wanaosafiri zaidi ya kilomita 8 kwa malori ya mchanga na mawe kwenda  Shule ya Sekondari  Fumagila.

Kitendo hicho cha wananchi kuvamia eneo hilo kimewafanya viongozi wa kata hiyo na uongozi wa shule hiyo kuwahadhari kusitisha haraka ujenzi huo, huku kukiwapo na mvutano kwamba halmashauri  ya jiji imeshindwa kutoa fidia kwa waliokuwa wamiliki wa ardhi hiyo na kuamua kuuza kwa wanaojenga sasa.

Wakizungumza katika mkutano kati wa  wananchi, Diwani wa Kata ya Kishili, Thobias Ndumi na Mtendaji wa kata hiyo,  Sayenda Mvanga, walisema wameshtushwa na taarifa kutoka kamati ya shule juu ya uvamizi huo na kulazimika kutembelea eneo hilo.

Kwa upande wa Mvanga, alitoa agizo kwa wakazi ambao wamejenga nyumba zao kutoziendeleza  na hata kuzibomoa wenyewe kwa kuwa eneo hilo ni la taasisi ya umma, licha ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokamilisha fidia kwa wamiliki wa eneo hilo ambao wameamua kuliuza kwa wengine ambao wanajenga sasa.

“Tayari tumeanza kuchukua hatua, naombeni hili tusilaumiane, hatuwezi kuona shule inavamiwa tukae kimya kwa sababu eti fidia haijatolewa, sote ni mashahidi maeneo yote ya hapa yaliyopimwa yameanza kufidiwa, tumeanza makaburi na tutaendelea kulipa kidogo kidogo kulingana na bajeti  inayotengwa,” alisema Mvanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles