33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

DC SONGWE APIGA MARUFUKU NAFAKA KUTENGENEZA POMBE

Na ELIUD NGONDO


dscf0310

MKUU wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Irando amepiga marufuku nafaka kutengenezea pombe wilayani humo.

Alisema hatua hiyo itawezesha  kutunza chakula cha kutosha   na kukabiliana na janga la njaa.

Alikuwa akizungumza na  wananchi wa Kata ya Chilulumo Tarafa ya Kamsamba.

Irando alisema  wananchi wamekuwa wakitumia nafaka nyingi kutengenezea pombe za kienyeji bila kujali kama wana chakula cha kuwatosha.

Alisema pombe za kienyeji zinatumia nafaka nyingi hususan  mahindi na ulezi.

Dc alisema kwa sababu hiyo  wananchi wanatakiwa kuacha kutumia nafaka kwa vile hali hiyo inaweza    kusababisha baa la njaa kipindi mazao yakiwa hayajakomaa.

“Ni marufuku utengenezaji wa pombe za kienyeji kwa kutumia nafaka.

“Mwaka huu kutokana na taarifa za watalamu wa hali ya hewa, inaonekana mvua itakuwa kidogo na kunaweza kukawa na baa la njaa,” alisema Irando.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Hiyo, Mathew Chikoti, aliwaasa wananchi kuwa na utaratibu wa kuweka akiba ya chakula wakati wa mavuno na kutokuuza ovyo.

Alisema hatua hiyo itawawezesha  kukabiliana na baa la njaa wakati mazao mengine bado hayajakomaa.

Alisema wananchi wanatakiwa kulima mazao yanayostahimili ukame na yanayowahi kukomaa kutokana na taarifa ya kutokuwapo kwa mvua ya kutosha.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Momba Adrian Jungu alisema yeye   na wataalamu wake watahakikisha wanasimamia   pembejeo ziwe katika ubora na wananchi wasipate shida wakati wa msimu   wa kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles