26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Lionel Messi awaliza mashabiki Argentina

DV1799611BUENOS AIRES, ARGENTINA

NYOTA wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, amewaliza baadhi ya mashabiki juzi, baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la dunia 2018 dhidi ya Colombia kwenye Uwanja wa Estadio del Bicentenario San Juan.

Nyota huyo alitangaza kustaafu soka la timu ya taifa mapema mwaka huu, baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa taji la Copa America dhidi ya Chile, kauli yake ya kustaafu iliwaliza wengi, huku baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wakimtaka abadili maamuzi hayo.

Baada ya muda alibadili maamuzi yake na kuanza kuitumikia timu hiyo, hata hivyo alionekana kucheza chini ya kiwango kutokana na kuwa majeruhi, lakini juzi alionesha uwezo wake na kuwafanya baadhi ya mashabiki kulia kwa furaha.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Argentina kushinda mabao 3-0, Messi aliweza kufunga bao la kwanza katika dakika ya 10 kwa mpira wa adhabu ambao aliupiga nje ya 18 na kuzama moja kwa moja wavuni.

Mbali na kufunga bao hilo, lakini mchezaji huyo alionesha kiwango cha hali ya juu, huku akitoa pasi mbili za mwisho ambazo zilizaa mabao mawili na kumfanya mchezaji huyo ashiriki katika kila bao.

Mashabiki walionekana kuwa na furaha ya hali ya juu kila wakati mchezaji huyo akipambana na wapinzani wake, hivyo baadhi ya mashabiki walionekana kutaka kupanda kwenye waya ambazo zimezungushwa uwanjani hapo, huku wengine wakifuta machozi yenye furaha.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mchezo huo juzi, mlinda mlango wa Colombia na klabu ya Arsenal, David Ospina, aliweka wazi kuwa hakuna njia sahihi ambayo wanaweza kuifanya Colombia kwa ajili ya kumzuia mshambuliaji huyo wa Argentina.

“Hakuna njia tunayoweza kuitumia kwa ajili ya kumzuia Messi asifanye lolote, tunaujua uwezo wa mchezaji huyo, tunajua nini lengo lake katika timu yake ya taifa.

“Hatuna jinsi lakini tunatakiwa kupambana kwa ajili ya kuona jinsi gani tunaweza kumzuia mchezaji huyo asiwe na madhara makubwa, hata hivyo tunatakiwa kupambana dhidi ya Argentina na si Messi peke yake kwa kuwa timu hiyo ina wachezaji wengi wenye vipaji,” alisema Ospina.

Michezo mingine ambayo ilipigwa juzi katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni pamoja na Chile ambayo ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Uruguay, huku Brazil ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Peru na Costa Rica ikishinda mabao 4-0 dhidi ya United States.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles