32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Rombo waishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja

Na Safina Sarwatt, Rombo

Wananchi wa vijiji vya Wama, Msangai na Nanjara Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameondokana na adha ya ukosefu wa daraja katika Mto Wama hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli za uzalishaji mali kipindi cha mvua.

Tayari Selikali imekamilisha ujenzi wa daraja hilo uliogharimu Sh million 131.5.

Aidha, kukamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji vya Wama, Msangai na Nanjara wilayani hapo, utawarahisishia wananchi kupata huduma bora kwa wakati, ambapo kipindi cha mvua wanafunzi wanalazimika kuacha shule na wajawazito walivushwa kwa kubebwa.

Wakizungumza wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipofika kuzindua daraja hilo, baadhi ya wananchi wamesema kukamilika kwa daraja hilo itawasaidia kufanya shughuli zao kwa uhuru bila kuhofia usalama na kwamba watakuwa wanatumia usafiri wa magari.

Lilian Kimario amesema awali daraja hilo ilijengwa kwa miti jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wananchi.

“Wagonjwa hasa mama wajawazito, walilazimika kuwavusha kwa mikono kwenda upande wa pili yalipo magari na hata kama ni msiba ilibidi tutafute utaratibu mwingine au kuzunguka mbali kusafirisha maiti,” amesema.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa daraja hilo, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Rombo, Rickson Lema amesema daraja hilo litarahisisha mawasiliano katika vijiji hivyo na kuimarisha huduma za kijamii.

Amesema mradi huu wa daraja la Mto Wama umegharimu Sh milioni 131.5 na kukamilika kwa mradi huu kumeimarisha huduma za usafiri na usafirishaji.

Akizindua daraja hilo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim amesema wameridhishwa kwa upande wa nyaraka na mradi wenyewe ambapo ubora na viwango vimezingatiwa.

“Baada ya kupokea taarifa ya kina na kuukagua mradi huu, tumejiridhisha kwa upande wa nyaraka pamoja na mradi wenyewe, ubora na viwango vimezingatiwa,” amesema Kaim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles