28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapokea Dozi 376, 320 za chanjo ya Moderna

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea Chanjo za UVIKO 19 Dozi 376,320 aina ya Moderna ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha inawakinga Wananchi wake dhidi ya ugonjwa huo.

Hafla fupi ya mapokezi imefanyika leo Desemba 24, 2021 na kuongozwa na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam  na kuhudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali, Ubalozi na Taasisi zisizo za kiserikali pamoja na viongozi wa CHAKUA (Chama cha Kutetea Abiria) ambao ni Wadau muhimu kwenye mapambano ya UVIKO-19 wakiongozwa na Mwenyekiti wao Taifa, Hassan Mchanjama.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Gwajima amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imelenga kuwakinga jumla ya Watanzania 188,160 kutokana na chanjo zilizopokelewa kupitia Mpango wa COVAX Facility ikiwa ni awamu ya kwanza kupokea aina ya chanjo hizo za Moderna.

“Mapokezi ya chanjo hizi za leo yanafanya jumla ya chanjo tulizopokea hapa nchini tangu tuanze kutoa chanjo za chanjo dhidi ya UVIKO-19 hadi sasa kufikia dozi 6,408,950 zikijumuisha (Sinopharm, Janssen, Pfizer), na leo Moderna ambazo zinatosha kuchanja jumla ya watanzania 3,204,475 hivyo niwaombe wanaohusika na zoezi hilo kuwajibika kwa kasi kubwa ili kuwawezesha watanzania wengi kupata chanjo mapema iwezekanavyo amesema Dk. Gwajima.

Aidha, Dk. Gwajima amesema kuwa Wizara imetoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania ili kudhibiti ugonjwa wa UVIKO-19.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles