27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia awakmumbuka wakazi wa kituo cha wasioona cha Buigiri

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi mbalimbali kwa wakazi wa kituo cha wasioona cha Buigiri-Matembe Bora,kilichopo  Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Wakazi hao ambao wapo jirani na makazi ya Rais Samia (Ikulu ya Chamwino) wamepokea msaada wa mbuzi, mchele,maji, maharage, sukari,sabuni ya unga na ya vipande, mafuta ya kupikia na vinywaji baridi zikiwemo Juisi na Soda.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 24,2021 katika kituo hicho, kwa niaba ya Rais mara baada ya kukabidhi zawadi hizo,Kaimu Mkurugenzi Huduma za Ikulu, Daniel Mwalusamba, amesema Lengo la zawadi hizo ni kushiriki pamoja na makundi maalumu katika kusherehekea sikukuu za Kristmas na Mwaka mpya pamoja na Rais kusheherekea kwa pamoja na majirani zake hao.

“Hawa ni majirani zake na Zawadi hii ni sehemu ya salamu za Krismasi ambayo imetolewa na mama yetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwajali Watu wenye mahitaji maalumu,”amesema Mwalusamba.

Mwalusamba pia amesema, Rais Samia anawatakia heri ya sikuu njema na kwamba wanapaswa kusherehekea kwa amani na utulivu.

Vilevile, ametoa  wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji maalumu katika kipindi hiki cha Sikukuuu ikiwa ni ishara ya kuwaenzi hali itakayowatoa kwenye upweke.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo hicho, Yared Cheleso, amemshukuru Rais Samia kwa zawadi hizo na kueleza kuwa huo ni upendo unaopaswa kuigwa na Wadau wengine huku akimtakia heri ya Afya njema na  utendaji mwema wa kazi.

Mbali na hayo wamemtoa hofu Rais kwamba wapo pamoja katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na hayuko peke yake bali wao pia wapo nyumba yake kwa Kila hatua.

“Wewe ni mama yetu,tunakuamini endelea kufanya kazi na sisi tupo nyuma yako,katika mapambano haya ya uvico 19 tupo pamoja na tunajitahidi kufuata hatua zote za kujikinga na kuwaelimisha wengine,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles