31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima: Tanzania ipo tayari kushirikiana na WB

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, amemhakikishia Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Dunia na Mkurugenzi wa Masuala ya Maendeleo ya watu kwa Nchi za Tanzania, Zambia, Malawi na Zimbabwe kuwa, Tanzania ipo tayari kushirikiana na Benki ya Dunia katika kutekeleza Afua ya Chanjo, wakati Dunia inapokabiliwa na Ugonjwa wa Covid-19.

Dk. Gwajima amebainishahayo katika kikao cha majadiliano kati yake na Mwakilishi wa Benki ya Dunia yaliyofanyika leo Alhamisi Desemba 24, 2021 katika ofisi za wizara ya afya jijini Dar es salaam.

Amesema Wwzara ya Afya imeanzisha mkakati wa kushirikisha vyombo vya habari, viongozi wa Dini, Wanasiasa, Watu maarufu kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi ili wapatiwe chanjo ya uviko-19 wakiwa kwenye maeneo yao.

“Kwa sasa tupo katika awamu ya Pili ya Mpango Shirikishi na Harakishi kwenye Masuala ya kupambana na Covid-19, ambao tuliuzindua mkoani Arusha Kaskazini mwa nchi yetu Desemba 22, 2021, na Maelekezo yamekwenda kwa wakuu wa Mikoa, na Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambao kwa pamoja wanashirikiana kwa karibu zaidi na wananchi katika kutoa elimu ya chanjo kwakuwatumia watoa huduma kwenye ngazi ya msingi kisha kupatiwa chanjo” amesema Dk. Gwajima.

Kwa upandewake Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Dunia na Masuala ya Maendeleo ya Watu katika nchi ya Tanzania, Zambia,Malawi na Zimbabwe Bw. Inaam Ui-Haq amesema kuwa benki ya Dunia imeonesha utayari kwa Tanzania katika uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu na kusaidia masuala ya Chanjo ya Uviko 19, Mama na Mtoto, ili kuweza wananchi kupata dawa kwa wakati pindi wanapofuata huduma katika vituo vya Afya.

“Benki ya Dunia, tupo tayari kusaidia Tanzania, lakini vema likapatikana andiko la juu ya Uviko -19, Pamoja na masuala ya Mama na Mtoto, kwa maeneo ambayo kama nchi inaona ni muhimu kuyaangazia kwa upekee” amesema Inaam Ui-Haq, ambaye ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles