29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Handeni yakabidhi madarasa ya Uviko-19

Na Mwandishi Wetu, Handeni

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amekabidhiwa madarasa manne katika Shule ya Sekondari Kwamatuku na Shyle ya Juu ya Handeni Girls zilizopo wilayani hapa yaliyojengwa kwa fedha za Uviko-19.

Aidha, amezipongeza kamati za ujenzi wa madarasa hayo yaliyojengwa kisasa kwa kusakafiwa na tiles kwa usimamizi mzuri wa fedha za serikali.

Kutokana na hatua hiyo, Handeni inakuwa wilaya ya kwanza kukabidhi mradi wa ujenzi wa madarasa hayo kwa Mkoa wa Tanga yakiwa yamekamilika.

“Nimefurahi kwa kuwa shule na kamati zenu mnasimamia fedha hizi kwa umakini mkubwa, unajua kwenye matumizi ya fedha za umma kila mara tunakwenda na kurudi nyuma.

“Kama mtakumbuka enzi hizo mambo yalivyokuwa serikalini, ili upate darasa kama hili zingeshapigwa si chini milioni 100, lakini leo tunahimizana Sh milioni 40 imetoa kitu kizuri namna hii, hiyo peke yake maana yake ni kwamba sisi kama wananchi tumeanza kujifunza misingi mizuri ya usimamizi wa fedha zetu wenyewe.

“Ile dhana kwamba mnasimamia mradi wenu mnatoa darasa kama hili ni kitu cha kupongezwa kwa sababu mimi nilikuwa Wizara ya Fedha, najua. Matumaini yangu ni kwamba huko mbele mtafanya maajabu na kwa sababu kipenzi chetu Mama Samia Suluhu Hassan anataka kumwaga fedha nyingi kwenye sekta ya elimu, afya na maji, hii nidhamu ya kusimamia fedha zetu tuwe nayo. Niwaambie ukweli, nimependa nilichokiona,” amesema Malima.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kwamatuku, Madilindi Madilindi amesema madarasa hayo yataondoa kero ya michango kwa wananchi hasa kipindi hiki cha msimu wa kilimo na mwisho wa mwaka ambapo mahitaji ya familia ni makubwa.

“Pamoja na mambo mengine, yataondoa adha ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kuripoti kwa awamu na msongamano wa wanafunzi madarasani lakini pia itaboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia na matokeo yake ni kuboreka kwa ufaulu na kujikinga kikamilifu na mlipuko wa ugonjwa wa corona,”amesema.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Handeni Girls, Mwajabu Hussein amesema anashukuru nguvu ya katika ujenzi wa madarasa hayo ambapo walishiriki kikamilifu kuchimba msingi na kuokoa Sh 200,000 ambayo ingelipwa kama kazi hiyo ingefanywa na fundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles