22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Diaspora: Tumerudi nyumbani kuwekeza kwenye mkonge

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ameitaka Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) kuwapatia Watanzania wanaoishi nje ya nchi, Tanzania Diaspora Hub (TDH) ekari 500 ili wawekeze kwenye kilimo cha mkonge.

Malima ametoa kauli hiyo Desemba 22, 2021 wilayani Muheza mkoani hapa, wakati alipokutana na Wanadiaspora hao ambao wameonyesha nia ya uwekezaji kwenye kilimo cha mkonge.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima(Kulia) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Saddy Kambona

Amesema uamuzi waliofanya ni kubwa kwa sababu malengo ya kitaifa ni kufika tani 120,000 ambayo imeipitiwa upya ifike sasa tani 100,000 ndani ya miaka minne hadi mitano ijayo na mikakati hiyo imeshaanza kwenye shamba la mbegu la Mlingano na wilaya zote za Tanga ambapo kumezalishwa vitalu mbalimbali.

“Tumezungumza nao katika mkakati huo, Mkoa wa Tanga peke yake tuwe na tani 65,00 kwa sasa tunazalisha tani 28,000 kwa hiyo tumezungumza na watu wa Bodi ya Mkonge tupate shamba la kama ekari 500 na uwekezaji wake uanze mara moja ili baada ya miaka minne, mitano hivi shamba la TDH liwe linaongezea tani 1,000 zaidi kwenye mkakati wa kuzalisha mkonge.

“Nimefurahishwa na hatua ya Diaspora kuwekeza nyumbani, hata Mungu amesema zungukeni katika dunia yangu mtafute riziki, kwa hiyo hata walioko China na kote duniani lakini nyumbani kwao ni Tanzania. Kitendo cha kusema tumepata hiki ebu tuwekeze ntyumbani hili linanipa faraja sana.

“Mimi mwenyewe nimewahi kuwa mwanachama wa Diaspora lakini sikuwahi kukumbuka katika miaka hiyo takribani 20 kuliwahi kutokea mtu mwenye akili hiyo ya kusema tuunde jambo ili tuwekeze nyumbani hakuna kwenye jambo lolote la maendeleo,” amesema Malima.

Pamoja na mambo mengine, Malima amesema amefurahishwa na hatua ya TDH kwamba nia yao si kuzalisha mkonge na kuuacha tu bali kuuongezea thamani kwa hiyo wanatarajia wataongeza thamani kwenye bidhaa kama kamba ambazo ndiyo jambo la asili, mkonge kama dawa, kinywaji, chakula cha mifugo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Saddy Kambona amesema kulingana na maelekezo ya serikali ya kuzalisha tani 120,000 kutoka tani 37,000 mwaka 2025, ambapo katika kufikia malengo hayo bodi imeunganisha nguvu za watu wengi zaidi kuingia kwenye kilimo cha mkonge.

“Kwa ndugu zetu wa TDH kwa sasa tutawonyesha hizo ekari 100 lakini malengo yetu ni kuwapatia ekari 2,000 ili waweze kuongeza mchango katika uzalisha si tu kwa Mkoa wa Tanga bali nchi kwa ujumla wake.

“Tunaamini wamefanya kazi nje ya nchi kidogo nguvu zao zitakuwa kubwa hivyo watumie hiyo nguvu yao kuja kuwekeza nyumbani kuchangia ongezeko hilo la uzalishaji kutoka tani 37,000 hadi 120,000,” alisema.

Naye Rais wa TDH, Nassor Basalama alisema kabla ya kuamua kuja kuwekeza nchini, wamezingatia uwekezaji mpana wa maeneo mbalimbali lakini kwa Tanga wameamua kwekeza kwenye mkonge na kilichowavutia zaidi ni bidhaa ambazo zinapatikana kwenye zao hilo.

“Tumeona bidhaa tofauti zaidi ya 50 ambazo zinaweza kuzalishwa na mkonge na kuongeza thamani yake na kuwa na kilimo kipana zaidi lakini hatujafikia huko.

“Kwa hiyo nadhani kuna fursa pana kupitia kilimo hiki na kukiongezea thamani vile vile kutoa fursa kwa wenzetu na serikali pia ifaidike na kwa kuwa tunao uwezo wa uwekezaji mpana kwa hiyo nadhani ni uwekezaji sahihi, mkonge ni kilimo cha kihistoria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles