SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limeanza uchunguzi dhidi ya mashabiki walioonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya mastaa wa timu ya taifa ya England, Raheem Sterling na Jude Bellingham.
Hatua hiyo inakuja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, kuitaka Fifa kuchukua hatua kali dhidi ya wale waliowabagua wachezaji hao jana, wakati England ‘ikiiua’ Hungary kwa kichapo cha mabao 4-0.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter, Johnson aliandika: “Ni jambo lisilokubalika kabisa kwamba wachezaji wa England walifanyia ubaguzi wa rangi nchini Hungary usiku wa jana.”
Hata hivyo, ilishangaza kuona Hungary ikiingiza mashabiki wake uwanjani, licha ya Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) kuizuia kufanya hivyo kwa mechi tatu.