23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

‘Ronaldo ametuvunjia heshima’

WAKONGWE wa Juventus, Sergio Brio na Alessio Tacchinardi, wameungana kumjia juu Cristiano Ronaldo wakisema ameivunjia heshima na kuiweka kwenye wakati mgumu klabu hiyo.

Akimzungumzia Ronaldo aliyerejea Manchester United, Brio aliyeichezea Juve mechi 385 kuanzia mwaka 1978 hadi 1990, amesema: “Juventus inastahili heshima. Sikutarajia kuona Ronaldo akiipuuuza kama vile. Halikuwa jambo zuri.”

Kwa upande wake, Tacchinardi amesema uondokaji wa Ronaldo ulishangaza zaidi kwa kuwa haukujali ukubwa wa klabu aina ya Juve.

“Ronaldo hakupaswa kuondoka vile. Isingekuwa kwa kuchukua ndege yake binafsi wakati kocha Allegri akizungumza na wachezaji kuelekea mechi dhidi ya Empoli,” amesisitiza Tacchinardi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles