28.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

Watoto wa kiume waongoza kuzaliwa Mwaka Mpya

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATOTO 49 wamezaliwa wakati wa shamrashamra za kuupokea mwaka mpya 2019 jijini hapa.

Watoto hao ambao kati yao 30 ni wa kiume na 19 wa kike, walizaliwa katika Hospitali za Rufaa za mikoa ya Mwananyamala, Amana, Temeke pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza na MTANZANIA jana, muuguzi wa zamu wa Amana, Gordian Chatanda, alisema hospitalini hapo walizaliwa jumla ya watoto 26 usiku huo wa mkesha wa mwaka mpya.

Chatanda alisema kati ya watoto hao 19 ni wa kiume huku saba wakiwa ni wa kike.

“Hakuna hata mmoja aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji, wote walizaliwa kwa njia ya kawaida, afya zao ni nzuri pamoja na mama zao,” alisema Chatanda.

Naye muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema walizaliwa watoto 11 hospitalini hapo.

“Watoto sita kati ya hao ni wa kiume na watano wa kike, watoto 10 walizaliwa kwa njia ya kawaida, mmoja tu ndiye ambaye alizaliwa kwa njia ya upasuaji,” alisema muuguzi huyo.

Aidha muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Temeke, Amos Henry alisema walizaliwa jumla ya watoto sita hospitalini hapo usiku huo.

“Watatu ni wa kike na watatu ni wa kiume, mmoja alizaliwa kwa upasuaji na wengine watano kwa njia ya kawaida,” alisema Herman.

Naye Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo alisema walizaliwa jumla ya watoto watano, kati ya hao wawili ni wa kiume na watatu ni wa kike. 

“Watoto watatu wamezaliwa kwa njia ya upasuaji na wengine wawili kwa njia ya kawaida, watoto pamoja na mama zao wote wanaendelea vizuri,” alisema Mwangomo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,646FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles