23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Fayulu akataa mwito wa maridhiano wa Tshisekedi

KINSHASA, Congo DRC

KIONGOZI  wa  upinzani nchini hapa, Martin Fayulu amekataa juhudi za Rais mpya,  Felix Tshisekedi za kutaka maridhiano, baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa kidemokrasia kumalizika.

Mwito huo wamaridhiano ulitoleawa na Rais huyo  mpya katika jitihada za kutafuta maridhiano ya kisiasa nchini hapa.

Hata hivyo jitiahada hizo za Rais Tshisekedi zinaonekana kugonga mwamba baada ya  Fayulu kusema kuwa  pale unapopewa mkono ambao ni mchafu, hupaswi kuupokea.

Kauli ya Fayulu imekuja siku chache baada ya Rais  Tshisekedi kusema katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kuapishwa kwamba  nchi yake haitakuwa ni ya upande mmoja ama ukabila, huku akisisitiza kuwa tayari kukutana na wapinzani ili waweze kushirikiana kujenga Congo imara.

“Tunataka kujenga Congo imara  katika utamaduni wake. Tutakuza maendeleo  kwa amani na usalama. Congo ni ya kila mmoja  ambapo kila mtu ana nafasi yake mwenyewe, “alisema Tshisekedi.

Fayulu alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano wake wa kwanza  tangu aliposhindwa kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wakati akiwahutubia  mamia ya wafuasi wake waliokusanyika mjini hapa.

Hata hivyo pamoja na kukataa wito huo wa maridhiano, kiongozi huyo aliwataka wafuasi wake wasifanye fujo wakati anapoendelea kupinga uchaguzi anaodai ulikumbwa na udanganyifu.

“Hakuna haja ya kufanya vurugu ila tutaendelea kupaza  sauti zetu katika jumuiya za kimataifa ili haki ipatikane,”alisema kiongozi huyo.

 Aliuhimiza Umoja wa Mataifa (UN) na wa Afrika (AU) kutopokea maagizo kutoka kwa mtu anayedai kuwa Wakongo hawakumchagua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles