25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA, IMEKUWA ZILIPENDWA?

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


KUNA kipindi niliandika kuhusu changamoto anazopitia kocha wa Yanga, George Lwandamina, nikaambulia matusi na maneno ya kuudhi yakanifanya nisirudie tena kumzungumzia, binafsi au Yanga.

Lakini mahaba ya mchezo wa soka yamenirudisha tena, ukweli ni kwamba muda wa viongozi wa Yanga, kusikia kilio cha mashabiki na wanachama wao dhidi ya kocha Lwandamina umefika.

Ukweli ni kwamba Lwandamina kashindwa kabisa kuiendesha Yanga, badala yake kaifanya icheze kama timu inayojilinda kushushwa daraja.

Kushindwa kwake kumesababishwa na vitu vingi pale Yanga kabla ya kumtaka aondoke, tuanze kujadili mazingira ya kazi yake kama inaruhusu kuwa na ndoto zozote.

Msimu uliopita ambao Lwandamina, alikabidhiwa timu hiyo katikati ya msimu alimalizia mafanikio ya Hans Van Pluijim kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, tukaona atakuwa kocha mzuri, msimu huu umeaza lakini bado thamani ya uwepo wake pale Yanga, haionekani hata kidogo.Nikisema hata kidogo nieleweke.

Ushirikiano wa Juma Abdul, Haruna Niyonzima na Simon Msuva upande wa kulia, haupo tena kwa sababu Niyonzima na Msuva  wameondoka.

Pia ushirikiano wa Haji Mwinyi, Deusi Kaseke na Thaban Kamusoko upande wa kushoto haupo, sababu Kaseke ameondoka.

Ushirikiano kwa wachezaji hao hasa upande wa kulia, ndio ilikuwa injini waliyokuwa wakiitumia Yanga na  kuwafanya Donald Ngoma, Hamis Tambwe na Obrey Chirwa kufunga mabao wanavyotaka.

Lakini mbadala wa wachezaji hao walioondoka ni Juma Mahadhi, Yusuph Muhilu kulia na kushoto ni Emmanuel Martin, Geofrey Mwashiuya, ambao wameshindwa kufanya kama tulivyowazoea msimu uliopita.

Sina shaka na wachezaji wapya  waliosajili hivi karibuni kama  Papy Kabamba Tshishimbi, Gadiel Michael, Rafael Daud, Youthe Rostand, Ibrahim Ajib na wengine,

Hivi ni kweli mbadala wa Vicent Bosou ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’?,  hapa Yanga ilikosea na inatakiwa kujisahihisha kwa kusajili mtu wa uhakika.

Enzi za Plujim timu ilikuwa vizuri kifedha,tukumbuke Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manjia bado alikuwa anaisaidia kwa hali na mali.

Kukosekana kwa fedha, ndio sababu ya morali ya wachezaji kushuka na si siri tena kwa sababu timu inashida ya kipesa.

Lwandamina ndo kocha pekee hivi karibuni, ambaye anapita katika kipindi kigumu hasa migomo ya wachezaji ya hapa na pale,lakini bado timu haijafungwa zaidi ya sare.

Kwa jinsi timu ilivyo kifedha hatuwezi pata kocha bora na mzalendo, wazungu wanaomsema usemao ‘Expensivity reflect the quality’ je tunayofedha ya kuajili kocha wa kiwango tunachokiitaji?.

Kwani hata kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa bado hakustahili kuwa kwenye nafasi hiyo, sababu hajathibitisha  ubora katika timu ya vijana.

“Vikombe vitatu hatujaridhika navyo tunataka tujichukuliage tu.Viongozi toeni mtu wenu.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ananiumiza akili yangu hata Lwandamina nae aniumize aaah jamani Mkwassa mbona hivyo eti,” hizo ni baadhi ya kauli za mashabiki wa Yanga.

Kwa sasa mashabiki wa Yanga wamejigawa makundi, kuna wanaotaka  Lwandamina afukuzwe na wanao mtetea abaki.

Lakini ni muhimu kufahamu kwamba watu waliofanikiwa duniani ni wale waliopitia kwenye machungu ya aina mbalimbali. Kuna wakati walishindwa, wakaumizwa na kupoteza matumaini,lakini hawakukata tamaa, wakajituma na wakafanikiwa.

Watu hawa wana shukrani, wapole, wakarimu na wanaelewa maisha yaliyowajaza ukarimu, upole na upendo. Watu hawa hawatokei tu bali ujifunza kupitia hali yao.

Yanga inapita katika kipindi kigumu sasa nje na ndani ya uwanja, ambapo ni dhahiri Lwandamina anawataka wadau wa klabu hiyo wawe na tabia kama za watu waliofanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles