23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AWAFUNDA WAZAZI KUSAIDIA WATOTO

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana, Anthony Mavunde, amewataka wazazi na walezi kuwasaidia watoto wao wanaosoma kwa kuhakikisha wanakagua madaftari yao ili wapate elimu bora itakayowasaidia katika maisha yao.

Kauli hiyo ilitolewa  mjini hapa jana na Salum Mkuya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa niaba ya Mavunde katika mahafali ya 4 ya Shule ya Sekondari ya Dodoma Central.

Alisema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa hawafuatilii maendeleo ya watoto wao hususani wanachofundishwa darasani kwa kuwaachia kila kitu walimu.

Alisema kufanya hivyo ni kosa kwani wazazi na walezi wanatakiwa kuwasaidia kwa kukagua madaftari yao pindi wanaporudi nyumbani ili kujua wamesoma nini katika siku husika.

“Elimu ndiyo msaada kwa watoto wetu kufanikiwa katika maisha yao, lazima tuwasaidie wazazi na walezi tuhakikisheni tunakagua madaftari ya wanafunzi  na mienendo yao…kuna watu wanaitwa oyaoya huwa wanawarubuni sana watoto wetu,” alisema.

Kuhusiana na wahitimu wa kidato cha nne, Mkuya aliwataka kuipenda nchi yao na kuhakikisha wanailinda na kupigania amani iliyopo na kuacha kufuata mkumbo kwenye mambo yasiyowahusu.

“Ipendeni nchi yenu izungumzeni kwa mambo mazuri achaneni na propaganda zozote zinazoendelea,” alisema.

Alisema katika siku za hivi karibuni, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), itaanzisha mafunzo ya wimbo wa Taifa kwa shule zote za Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Adiru Swaibu, alisema shule hiyo imejikita kutoa elimu bora itakayomsaidia mwanafunzi kujikwamua kisiasa, kiuchumi na kijamii.

“Shule yetu ni ya kidato cha kwanza mpaka cha sita na katika siku za hivi karibuni tutaanza kutoa mchepuo wa sayansi, tumekuwa tukifanya vizuri hata Waziri wa Elimu mwaka jana alitupatia cheti kama moja ya shule inayofanya vizuri,” alisema.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, Isaya Ruben alisema wamejiandaa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles