23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO WA HOSNI MUBARAK MBARONI

CAIRO, Misri


SERIKALI ya hapa inawashikilia watoto wawili wa kiongozi wa zamani, Rais Hosni Mubarak, kwa tuhuma za kukiuka kanuni za soko la hisa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la hapa, Mena, watoto hao wawili wa kiongozi huyo, Alaa  na  Gamal Mubarak, walikamatwa juzi wakikabiliwa na tuhuma hizo za ukiukwaji wa kanuni hizo za soko la hisa na za Benki Kuu ya nchi hii.

Shirika hilo la habari liliripoti jana kwamba kesi dhidi ya watuhumiwa hao ilianza tangu mwaka 2012, ukiwa ni mwaka mmoja baada ya baba yao kuondolewa madarakani na wawili hao walikuwa nje kwa dhamana kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kwamba wanandugu hao ambao wanakana makosa yao watafikishwa mahakamani Oktoba 20, mwaka huu.

Mbali na hao, Mahakama hiyo ya mjini hapa, pia imeagiza kukamatwa kwa watu wengine watatu walioshiriki kuhujumu pauni za hapa bilioni mbili.

Katika kesi hiyo, Alaa, 57 na Gamal, 54,  wanatuhumiwa kujipatia pauni za nchi hii milioni  494, baada ya kuamua kuuza Benki ya Taifa kwa ajili ya kujipatia faida.

Kwa sasa Alaa ambaye ni mfanyabiashara ameachana na masuala ya siasa wakati Gamal ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa benki ndiye aliyekuwa akiandaliwa kuwa mrithi wa baba yake kabla ya kutokea vuguvugu la mapinduzi katika nchi za Kiarabu mwaka 2011.

Wanandugu hao pia wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara kutokana na tuhuma mbalimbali na wameshavitumia vipindi kadhaa wakiwa rumande.

Kesi hizo ni pamoja na ya Mei 2015, wakati Alaa na Gamal Mubarak,  walipohukumiwa sambamba na baba yao kifungo cha miaka mitatu jela kwa kujipatia pauni milioni 125 za umma ambazo walidai kuzitumia kukarabati makazi ya rais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles