24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaohama vyama wanautaka ‘U-Waitara’-Kambaya

                  Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya amesema hamahama ya ya wabunge na madiwani wa upinzani kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM) wengi wao wanafuata maslahi binafsi na sio kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Kauli hiyo ya Kambaya imekuja siku moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF Abdallah Mtolea kujiuzulu ubunge na nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo ndani ya chama hicho jana Alhamis Novemba 15, bungeni jijini Dodoma na kutangaza kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa na migogoro ndani ya chama chake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CUF leo Ijumaa Novemba 16, Kambaya amesema chama hicho hakina mpango wala hakijaitisha kamati ya maadili na nidhamu ili kumjadili mwanachama yoyote si wiki ijayo wala mwezi ujao hivyo Mtolea aliamua kwa utashi wake mwenyewe kuhama na sio kwamba amesikia anataka kufukuzwa.

“Kuwa na mgogoro na chama hakuwezi kufanya uache ubunge kwasababu unapochaguliwa unaenda kufanya kazi ya wananchi na si chama, hivyo Mtolea kahama mwenyewe asisingizie alikosa ushirikiano.  

“Wengi wao wanaohamia CCM wanautaka ‘uWaitara’ kwa maana kuwa wanataka kuchaguliwa kushika nyadhifa serikalini kama kuteuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri  kama alivyoteuliwa mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, “ amesema Kambaya.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles