25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa bustani kutafutiwa masoko ya uhakika Lindi

HADIJA OMARY, LINDI

Serikali imewahakikishia vijana 18,800 wanaotekeleza mradi wa ulimaji wa bustani Kibiashara kupitia teknolojia ya kitalu nyumba  kuwatafutia masoko ya uhakika ya bidhaa zao ili kilimo hicho kiweze kuwa na muendelezo.

Mradi wa ulimaji wa bustani kwa kutumia teknolojia ya vitalu nyumba pamoja na ujenzi wa vitalu nyumba unatekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu  kupitia Programu ya Taifa ya kukuza Uchumi ambayo inaendeshwa katika Halmashauri  83 nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,  Ajira na Wenye ulemavu Atony Mavunde baada ya kutembelea na kukagua vitalu Nyumba vilivyojengwa na Vijana wa kijiji cha Mwananyamala Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea na kitalu cha vijana wa  Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani humo kilichopo Mtaa wa Ngongo Tulieni.

Mavunde amesema Lengo kuu la mradi huo ni kutoa mafunzo yatakayo wawezesha Vijana kupata ujuzi  wa kujenga kitalu nyumba pamoja na kulima bustani kwa kutumia teknolojia, hiyo ili kuongeza tija katika kilimo na kuvutia vijana wengi kujiajiri kupitia kilimo.

“Tumejipanga kuhakikisha wale wote wanaojihusisha katika sekta hii ya kilimo tuwasaidie  watoke hapa waende mbele zaidi  sababu aina maana kama serikali tukitumia fedha nyingi za walipa kodi kuwekeza hapa alafu hakuna muendelezo  malengo  na matarajio yetu ni kuwaunganisha vijana hawa na taasisi za serikali ikiwemo sido ili pia nao washiriki katika uchumi wa viwanda”  amesema.

Aidha amesema katika kulitekeleza hilo tayari Serikali imeshatafuta makampuni zaidi ya mawili ambayo yameshaanza kazi ya kutafuta masoko ya bidhaa hizo ndani na nje ya nchi ambayo yataunganishwa na vijana katika maeneo yao ili fedha ambayo inapatikana katika mauzo hayo iweze kuzunguka na kuwasaidia vijana wengine .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles