23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAHAMIAJI HARAMU 236 WAKAMATWA TANGA

Oscar Assenga, Tanga

Wahamiaji haramu 236 wamekamatwa mkoani Tanga kwa kuingia nchini bila kibali katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha Januari hadi Mei 16 mwaka huu.

Kaimu Ofisa Uhamiaji, Mkoa wa Tanga Salum Farahani amesema hayo leo Mei 16, wakati akizungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakiingia mkoani hapa kama njia kuelekea nchini Afrika Kusini.

“Wahamiaji hao walikamatwa kwa kipindi hicho kwa miezi tofauti tofauti ambapo 49 walikamatwa Januari, 77 walikamatwa Februari, 18 walikamatwa Machi, 26 mwezi Aprili huku 66 wakikamatwa kuanzia Mei mwaka huu.

“Idadi kubwa ya wahamiaji wanatoka nchini Ethiopia na ndiyo kundi kubwa linaloongoza kwa kukamatwa ambapo kwa kipindi hicho walikamatwa 140, wakifuatiwa ambapo wamekuwa wakifika nchini kwa kusafirishwa na Watanzania ambao nao waliokamatwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles