Imechapishwa: Sat, Aug 12th, 2017

UWANJA NJOMBE MJI WAKAMILIKA

 

Na MAREGES NYAMAKA-DAR ES SALAAM

UKARABATI wa Uwanja wa Sabasaba unaotumiwa na timu ya Njombe Mji umekamilika kwa ajili ya kutumika kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kutimua vumbi Agosti 26.

Akizungumza na MTANZANIA jana, meneja wa klabu ya hiyo, Boniface Damian, alisema tayari wamekabidhiwa uwanja huo na wahusika ambapo walianza kwa kuutumia jana kufanya mazoezi.

“Tumekabidhiwa tayari uwanja ambapo leo (jana) timu imefanya mazoezi ni jambo jema sana hili kwetu kwani umekamilika ndani ya wakati ili wachezaji waanze kuuzoea mapema kabla ya siku chache ligi kuanza,” alisema.

Alisema wanatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki ndani ya uwanja huo wiki ijayo dhidi ya Singida United na baadaye kuwafuata Majimaji ya Songea.

Njombe Mji wanaonolewa na Hassan Banyai akisaidiana na Mrage Kabange, watafungua pazia la Ligi Kuu  kwenye dimba lao hilo wakiwavaa Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

UWANJA NJOMBE MJI WAKAMILIKA