23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA

Na MWANDISHI WETU -MWANZA

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amekagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na ya kisasa itakayotoa huduma za usafirishaji katika  Ziwa Victoria.

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) jana jijini hapa, Profesa Mbarawa amewataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.

“Mkandarasi ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa kihesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi,” alisema Profesa Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv. Clarias na Mv. Umoja, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari  ya ‘Port Bell’ nchini Uganda.

“Kukamilika kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye biashara wakati wote na kuhakikisha kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha kujiendesha kwa faida,” alisema.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Erick Hamissi, amemhakikishia Profesa Mbarawa kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika Ziwa Victoria na Tanganyika.

“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika ubora unaostahili wakati wote,” alisema Hamissi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles