TRUMP: NIPO TAYARI KUKUTANA NA KIM KWA MARA YA TATU

0
415

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya mkutano wa tatu na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, huku akisisitiza kuwa Washington haitaviondoa vikwazo ilivyoviweka dhidi ya taifa hilo.

Trump amesea mkutano huo unaweza kufanyika, lakini si mchakato wa haraka bali ni wa hatua kwa hatua.

Amesema hayo kwa waandishi wa habari, mara baada ya kuzungumza na rais wa Korea Kusini, Moon Jae In ofisini kwake ambapo walijadiliana kuhusu uwezekano wa Moon kufanya mkutano wa kilele na Kim haraka iwezekanavyo, kama njia ya kuchochea mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu kuachana na silaha za nyuklia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here