TANESCO YAWAONYA WANAOCHOMA MOTO MASHAMBA

0
5

Wananchi na wakulima wanaosafisha mashamba yao baada ya mavuno kwa kuchoma moto, wametakiwa kuacha kitendo hicho ili kunusuru miundombinu ya Shirika la umeme (Tanesco), zikiwamo nguzo za umeme.

Meneja mradi wa umeme wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, amesema leo mjini Songea kuwa uchomaji huo wa moto umesababisha hasara kubwa kwa Tanesco na kulazimika kuzima umeme ili kuepusha madhara makubwa.

“Uchomaji moto mashamba katika moja ya mashamba hapa Songea umesababisha uharibifu wa nguzo za umeme ambao unakwenda kwenye shamba la Kahawa la Aviv la mjini Songea.

“Kuhusu mradi wa umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe unatarajiwa kumaliza tatizo la umeme na kuwa na umeme wa uhakika kwa vijiji 191,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, amesema hatua hiyo ya inakwenda sambamba na ujenzi wa njia ya umeme kutoka Makambako hadi Songea ambapo kazi hiyo pia inahusisha upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa Kilovolti 220/132/33Kv, na ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na Songea vya msongo umeme wa kilovolti 220/33kV, halikadhalika ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa hiyo.

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema ni vema wananchi watambue wana wajibu wa kulinda miundombinu ya umeme kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here