25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TAASISI ZA JESHI ZAPIGIWA DEBE ZAO LA KOROSHO

Na OSCAR ASSENGA-TANGA


BODI ya Korosho Tanzania (TCB) Mkoa Tanga, imeshauriwa kuzitumia taasisi za jeshi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT Mgambo na JKT Maramba  ziweze kusaidia katika uzalishaji wa miche ya korosho.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa Tanga, Martine Shigela kwenye mkutano wa wadau wa   korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya tasnia ya zao hilo kwa   miaka mitatu.

Shigella alisema ili bodi hiyo iweza kukabiliana na uhaba wa miche katika halmashauri zinazolima zao hilo, lazima taasisi hizo zipewe mbegu kwa ajili ya kuzalisha miche hiyo.

“Jaribuni kuwasiliana na taasisi hizo za jeshi ambazo zina wataalamu wa kuandaa vitalu na wanaweza kuwasaidia kuzalisha miche mingi na iliyo na ubora unaotakiwa.

“Pia, halmashauri zote zinazolima korosho lazima zihakikishe zinatenga bajeti mapema ndani ya mwezi huu wa Septemba kwa ajili ya ununuzi wa mbegu kutoka katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele kwa ajili ya kuzalisha  miche ambayo inatarajiwa kusambazwa mwakani kwa wakulima wote,” alisema Shigela.

Awali,   Meneja wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki, Ugumba Kilasa, alikiri umuhimu wa kuzitumia taasisi hizo kutokana na   uhaba wa fedha zilizokuwa zinatumika kuvilipa vikundi vinavyozalisha miche hiyo.

“Lengo ni kuwa na mjadala wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo mkoani hapa na ongezeko hilo lazima liende sambamba na kuwapo  miche mipya, bora na ya kisasa.

“Awali, tulikuwa na vikundi vya vijana tuliokuwa tunawatumia kuzalisha miche hiyo na tulikuwa tunawalipa.

“Lakini kutokana na ufinyu wa fedha ni bora tutumie taasisi hizo za JKT ambazo naamini zitatusaidia,” alisema Kilasa.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa Tanga, Jacklin Senzige, alisema kuna tatizo la upatikanaji wa pembejeo kwa wakati jambo ambalo alisema linaweza kukwamisha usambazaji wa mbegu hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles