23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAELEZA MIKAKATI YA ELIMU BURE

NA TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema inaandaa utaratibu wa watoto wa kike kuonyesha cheti cha kumaliza kidato cha nne (Leaving Certificate) ndipo wafungishwe ndoa.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika Kijiji cha Mfili wilayani Nkasi na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda.

Alisema kupitia sera mpya ya elimu wataweka kipengele cha kuzuia dhamana kwa atakayemwozesha mwanafunzi katika sheria itakayoandaliwa hivi karibuni.

“Tunakoelekea watoto wote watasoma shule za msingi na sekondari na ili aolewe atalazimika kuonyesha ‘Leaving Certificate’.

“Kama hajamaliza Form Four (kidato cha nne), OCD subirini wamalize kufunga ndoa, wakiingia ukumbini mlete karandinga na kuwasomba wote, peleka mahakamani,” alisema Kakunda.

Alisema kuwa adhabu ya kwenda jela miaka 30 itawagusa wote walioshiriki, akiwamo kiongozi wa dini atakayefungisha ndoa hiyo, wazazi wa pande zote mbili, aliyeoa na waliokwenda kushangilia.

“Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na ‘Leaving Certificate’ ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi,” alisema Kakunda.

Aliwataka kuchukua tahadhari kwa kupata taarifa sahihi kutoka katika shule aliyosoma binti ikiwa ni pamoja na kuona cheti cha kumaliza kidato cha nne.

Alisema kuwa kitendo cha kumkatisha mtoto wa kike  kumaliza masomo kwa sababu ya mimba ama kuozeshwa, ni jambo la kuudhi na limeendelea kuisumbua Serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike.

“Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa mkoa mzima jambo linaloisikitisha Serikali,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles