23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS PUTIN AFICHUA NJAMA ZA KUVURUGA UCHAGUZI

MOSCOW, Urusi

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kwamba, madai ya Marekani kuwa nchi yake iliingilia uchaguzi wao wa mwaka jana yana lengo la kutaka kuleta matatizo katika uchaguzi wao wa mwakani.

Taarifa hiyo imekuja wakati Shirika la Makachero la Marekani, FBI, likiendelea na uchunguzi ili kuangalia kama Serikali ya Moscow ilitia mkono katika uchaguzi huo ambao Rais Donald Trump aliibuka na ushindi.

Katika hotuba yake aliyoitoa juzi katika maadhimisho ya Wiki ya Nishati, Rais  Putin  alisema kwamba, nchi yake na Marekani zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya msingi, kama sera za kuimarisha nishati, kupambana na uhalifu wa kimtandao, kuzuia matumizi ya silaha za maangamizi  na jinsi ya kutafuta suluhu katika mgogoro wa Syria na mataifa mengine.

“Kwa kuwa wanataka kulipiza kisasi katika madai yao ya kwamba tuliingilia uchaguzi wa Marekani, naona wanataka kuleta matatizo katika uchaguzi wa Urusi,” alisema Rais Putin.

“Sisi na Marekani tumekuwa tukishirikiana vizuri katika masuala muhimu na yenye maslahi baina ya nchi hizi mbili na hatukuwahi kujiingiza katika uchaguzi wao,” aliongeza kiongozi huyo.

Alisema mbali na hilo, pia shutuma dhidi ya Serikali ya Moscow kuhusu kuunga mkono dawa za kusisimua misuli nayo ni njia mojawapo ya kutaka kuvuruga uchaguzi huo wa rais.

Hata hivyo, Rais Putin alielezea matumaini yake kuwa, masuala haya yote muhimu wanayoshirikiana yatasababisha uboreshaji wa mahusiano ya nchi hizi mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles